Maisha ya Office 2007 yafikia tamati ndani ya Microsoft

  812

  Kampuni ya Microsoft imetangaza rasmi kuachana na bidhaa zote za Office 2007 ifikapo Oktoba 10 mwaka huu.

  Microsoft iliandika, “Ifikapo tarehe 10 Oktoba mwaka huu, Office 2007 itafikia Mwisho wa Maisha. Kama bado hujaboresha Office 2007 yako kwenda kwenye matoleo mapya, unashauriwa kufanya hivyo sasa.”

  Mara baada ya maisha ya Office 2007 kufikia tamati, Microsoft hawatotoa huduma zifuatazo kwa watumiaji:

  • Msaada wowote wa kiufundi.
  • Kutatua masuala ya wadudu/bugs mara yatakapogundulika.
  • Kutoa msaada wa kiusalama katika mapungufu yoyote yatakayoonekana.

  Soma Pia: Njia nne za kufanya simu yako ya Android iwe haraka

  Microsoft imetoa ushauri ufuatao kwa watumiaji wa toleo la Office 2007:

  • Kuboresha (upgrade) kwenda Office 365 ProPlus.
  • Kuboresha kwenda Office 2016.
  • Kuboresha kwenda matoleo yoyote mapya baada ya Office 2007, kama Office 2013.