Playstation waleta gamepad kwa ajili ya watoto wanaocheza PS4

744

Hatua inayofata kutoka kwa watawala wa ‘console games’ ni kuwezesha urahisi wa uchezaji kwa wenye mikono midogo hasa watoto

Gamepad hiyo ina mvuto na umbile dogo kulingana na mkono mdogo, ni baada ya Sony kuungana na kampuni ya watengenezaji ‘hardware’ Hori kuleta toleo hilo.

Wameelezea pia gamepad hiyo ina ukubwa mdogo wa 40% kulinganisha na gamepad ya kawaida, haitakua na vitu kama mtingishiko(vibration), sehemu ya kuweka ‘earphones’, taa ya LED, ‘touchpad’ na ‘motion control’.

 

Soma pia:KRACK: Taarifa yatolewa simu janja hasa Android na kompyuta zote zenye Wi-Fi zipo hatarini

Itaanza kupatikana mwezi wa 12, na toleo la ‘exclusive’ ni rangi ya blue, bei za gamepad hizo itakua nusu ya gamepad za kawaida (dualshock 4).