Roboti Sophia akutana na waziri mkuu wa Ethiopia na kwenda maonyesho ya ICT

242

Sophia ni roboti aliyepata umaarufu na kupewa uraia wa Saudi Arabia, kwa uwezo wake wa kuongea, kujibu maswali, ishara za uso, na kusoma hisia za watu anaoongea nao.

Amewasili bara la Afrika nchini Ethiopia kuonana na Waziri mkuu Abiy Ahmed siku ya jumatatu na kuongea kuhusu misaada ya ubunifu wa teknolojia. Ingawa alipata hitilafu kidogo ya vipande vya mwili wake kupotea Airport wiki iliyopita. Ikafikia hatua ya kuahirisha mkutano na chakula cha usiku na waziri mkuu ijumaa iliyopita.

Soma Pia:ROBOTI SOPHIA: Saudi Arabia yampa roboti uraia kama binadamu wengine

Sophia ametengenezwa na kampuni ya kichina Hanson Robotics, na akapewa uwezo wa kuongea lugha ya Amharic ambayo ni lugha kuu nchini Ethiopia. Imekua ni lugha ya pili baada English.

Sophia atahudhuria maonyesho ya ICT yaliyo anza kuonyesha jumatatu nchini humo Ethiopia.