ROBOTI SOPHIA: Saudi Arabia yampa roboti uraia kama binadamu wengine

1559

Sophia ni roboti wa kwanza duniani kupewa uraia katika historia. Kwenye mkutano wa ‘Future Investment Initiative’ uliofanyika kwenye nchi ya kiarabu Saudi Arabia, ambapo roboti huyo alipewa nafasi ya kutoa hotuba na kujibu maswali

Ingawa Saudi Arabia ni nchi inayojulikana kwa unyimaji wa haki za wanawake, imeshangaza wengi kuumpa Sophia kipaumbele na kumtambua kama mwanamke mwenye uraia na haki zake.

Katika hotuba yake, roboti huyo alisema atatumia intelligence ya bandia (AI) kufanya maisha ya binadamu kuwa mazuri zaidi. Andrew Ross Sorkin kutoka CNBC akapata nafasi ya kumhoji maswali. Kwenye majibu yake, Sophia aliongea na kumtania Elon Musk ambae ni tajiri mkubwa anaejulikana kwa kuanzisha kampuni ya tesla na SpaceX, utani huo ni ulitokana na Elon Musk aliwahi kuongelea taaluma ya AI na roboti kuwa ina hatari kubwa kwenye miaka ijayo.

Angalia hotuba yake ya mkutano wa ‘Future Investment Initiative’ na alivyojibu maswali

Kwa ujumla tunaelekea kwenye dunia yenye intelligence ya bandia (AI), na makampuni makubwa mengi yanawekeza mabilioni ya pesa kwenye taaluma hiyo ya AI. Tuambie maoni yako kuhusu roboti Sophia mwenye uraia.