Samsung wagawa simu 200 za Galaxy Note 8 kwenye ndege

790

Sisi sote tunafahamu kua mwaka mmoja uliopita, watu wengi waliambiwa hawatoweza kusafiri na simu zao aina ya Samsung Galaxy Note 7 kwenye ndege zikiwa na kashfa ya kuungua moto. Hata hivyo, sasa kampuni ya Samsung yenye makao yake makuu nchini South Korea hivi karibuni wametoa zawadi ya simu za Galaxy Note 8 kwa abiria kwenye ndege ikiwa ni jaribu la kuuthibitishia dunia kua simu zake za Galaxy Note 8 ni salama.

Samsung wagawa simu 200 kwa abiria wote wa safari ya ndege

Kampuni ya Samsung iliwashangaza abiria 200 wa ndege ya Iberia IB514 iliyokua ikifanya safari kutokea A Coruna kuelekea Madrid kwa zawadi ya Galaxy Note 8 kwa kila mmoja, simu yao hiyo yenye thamani ya $1190 (TZS 2.6 million). Kwa mpango huu kampuni ya Samsung inachukua hatua nyingine katika harakati za kusaficha picha mbaya iliyojijengea kwenye toleo lao lililopita la Galaxy Note 7, ambayo ilitolewa sokoni na kukatazwa kabisa kwenye safari za ndege ikihofiwa ingeweza kusababisha moto ndani ya ndege.
Abiria waliopanda ndege ya Iberia walianza kushuku kua wanaweza kua ubao wa matangazo wakati wakikaribishwa na ujumbe unaosema “Welcome aboard Galaxy Note 8” ambayo kampuni hiyo ya Korea (Samsung) na kampuni ya ndege (Iberia) wamekua wakiizindua kwa kipindi cha wiki kadhaa zilizopita, na rubani alikwenda kwa abiria wote kuthibitisha walikua wahusika wa tukio hilo muhimu.
Baadhi ya matatizo ya toleo la Galaxy Note 7, yalikua battery zake zilikua zikiwaka moto hali iliyokua ikisababisha kuharibu kabisa kwa simu hizo, iliyopelekea kuharibu taswira ya kampuni hiyo kongwe. Makampuni ya ndege hayakuchukua muda mrefu kutoa matamko na mwezi Septemba mwaka jana, walikataza kabisa kwa abiria kupanda ndege na kifaa hicho.

 Je, unafikiri Samsung wanaweza kurudisha imani ya bidhaa zao kwa njia hii? Unaweza kutuachia maoni yako katika hili hapo chini.