Samsung wametangaza Galaxy S9 na hizi ndio sifa zake

872

Tofauti kati ya Galaxy S9 na Galaxy S8 sio kubwa, ila ni ndogo zenye ukubwa wake. Kwa nje muonekano unafana, hadi ujue mabadiliko mapya ndo utaweza kuzitofautisha

Katika kongamano huko mjini Barcelona, Samsung wametangaza Galaxy S9 na Galaxy S9+. Sifa yake kubwa ni Camera, AR Emoji, Bixby na uwezo wa simu.

Camera

Galaxy S9+ ndo simu ya kwanza na camera mbili katika matoleo ya Galaxy S. simu hizi mpya zinakuja na ‘Dual Aperture’ ya f/2.4 na f/1.5, itakayo boresha upigaji picha wako. Pia simu hizo mbili zinaweza kuchukua video ya slow-mo kwa uzuri zaidi, hii imetokana kwa kuongeza nguzu ua kurekodia had 960fps, ambayo kwa simu ni kubwa sana na pekee.

Tofauti ya Galaxy S9 na Galaxy S9+, ni kwamba Galaxy S9+ inakupa uwezo wa kupiga ‘Live Focus Portraits’ kutokana na kuwa na camera mbili, zinashirikiana kuboresha picha yako, kama ilivyo camera ya iPhone 8 Plus.

Galaxy S9 Plus Camera

AR Emoji

Samsung wamewalipa Apple(Animoji) kwa kuleta AR Emoji, camera itakupa uwezo wa kutengezea katuni anaefanana na sura yako, kurekodi ukiongea au kuimba. kisha utaweza kutuma kwa marafiki au kwenye mitandao ya kijamii.AR Emoji

Bixby

Sehemu nyingine iliyopewa mabadiliko ni kwenye msaidizi wa simu yako, imepewa teknolojia ya AR (Augmented Reality), kutafsiri lugha mubashara, chakula na sehemu ya vipodozi. Bixby inakupa uwezo kusoma maneno katika picha hapo hapo, kusomea maandishi yaliyoandikwa kwa mkono na kutafsiri. Pia ukiweka selfie kwenye Bixby uweza kuvalishwa make-up na utaweza kununua hivyo vipodozi kama utavitaka. Bixby inaweza kubashiri kalori za chakula chako kwa kuangalia kwa camera

Bixby, Personal Assistant

Soma Pia: Jinsi ya kuchagua kompyuta itakayofaa kutumia na aina za watumiaji

Vinginevyo

Samsung wamehamishia spika za stereo mbele na chini na kuifanya iwe na sauti kubwa mara 1.4 zaidi ya Galaxy S8. Galaxy S9 imepewa RAM ya 4GB na Galaxy S9+ imepewa RAM ya 6GB. Zote zitakuwa na Android 8.0 Oreo. Battery pia Galaxy S9 ina 3,000mAh wakati S9+ ina 3,500 mAh, zote zinazuia maji na kuwa na teknolojia ya wireless-charging.

 

Nini maoni yako kuhusu simu za Samsung ? tuandikie na kisha tutakujibu. Ahsante.