Samsung yawadhihaki iPhone katika tangazo lao jipya

835

Ushindani wa kibiashara kati ya makampuni ya simu za iPhone na Samsung umeendelea kupamba moto huku ukihusisha kutupiana vijembe ili kuweza kuvutia soko kwa kila upande wao.

Samsung ambao mara nyingi hupenda kuwadhihaki Apple na wateja wake kwa kupanga foleni ili kupata matoleo mapya ya simu za iPhone wamerudi tena kurusha vijembe kupitia tangazo lao jipya lililozungumzwa sana mitandaoni.

Kichwa cha tangazo hilo lenye urefu wa dakika moja ni “Growing Up” na kama linavyoonekana hapo juu, limerusha vijembe vya moja kwa moja kwa Apple iPhone na historia ya ushindani dhidi ya Samsung Galaxy.

Katika tangazo Samsung wanaonesha maumivu wapiga picha kupitia iPhone walipata mnamo 2010 kutokana na uwezo mdogo wa kuhifadhi vitu hususani walipojaribu kupiga picha na kupewa ujumbe wa “Storage Full”

Soma Pia: Samsung wagawa simu 200 za Galaxy Note 8 kwenye ndege

Tangazo pia linaonesha mvulana na msichana wakianguka ziwani mara baada ya msichana kupiga picha kupitia simu ya Samsung. Wakiwa wanatoka majini simu ya Samsung inaonekana ikiendelea kufanya kazi na ile ya iPhone ikiwa imekufa kutokana na kukosa kipengele cha kuzuia maji “waterproof”.

Mada kuu katika tangazo hilo ni kuonesha jinsi Samsung walivyo mbele siku zote dhidi ya Apple hususani katika masuala ya hardware na pia kuongeza chachu ya ushindani kati ya makampuni hayo ya simu.