Sasa Spotify imeanza kupatikana huko nchini Afrika Kusini

666
App Ya Spotify

Spotify imeachiwa na kuanza kutumika rasmi huko Afrika Kusini. Kwa Pamoja na watumiaji milioni 159, wa nchi zilizoendelea

Spotify ni mtandao wa kusikiliza muziki wa kila aina duniani kote, ambao unakuwezesha kutafuta na kutengeneza playlist za muziki wa kila msanii, mpaka sasa unanyimbo karibuni milioni 35. Ukitumia bure utaweza kusikiliza nyimbo bila gharama ila utapata matangazo ya hapa na pale, kama utapenda kulipia ni kiasi cha dola 9.9 kwa mwezi.

Soma Pia: Tigo yaungana na Selcom na Mastercard kuleta huduma ya Mastercard QR Tanzania

Mkurugenzi mkuu Michael Krause alisema ” Spotify wanafuraha kubwa kuachia huduma hiyo nchini humo Afrika ya Kusini. Tumekuwa tukiangalia bara hili jinsi ya kuwaletea huduma hii na kufanya waafrika wapate vionjo vya muziki wa aina zote, na bila kuwasahau wasanii waweze kuweka nyimbo zao kwa urahisi ili zipatikane duniani kote”

Kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania, bado haziwezi kutumia Spotify na kulipia huduma hiyo.

Nini maoni yako ?

Ongea na mimi kuhusu teknolojia kwenye Twitter