Shambulio: Mwanamke ajeruhi watu wanne katika shambulio, YouTube HQ

705
shambulio-youtube

Takribani wafanyakazi 1,700 katika makao makuu ya YouTube huko San Bruno, California, walijikuta shughuli zao zikikatishwa Jumanne, muda mfupi baada ya mashambuliaji kuvamia ndani ya jengo la kampuni hiyo na kuanza kuwapiga watu risasi.

Polisi katika eneo hilo walipokea simu kadhaa za dharura na kuelekea eneo hilo. Watu wanne walijeruhiwa katika shambulio hilo, na mwanamke aliyeshukiwa kuwa mashambuliaji (Nasim Najafi Aghdam) alikutwa baadae amefariki kwa kujipiga risasi.

SOMA PIA: Microsoft kumpa vifaa mwalimu wa Ghana anaefundisha kompyuta ubaoni

Wafanyakazi wa kampuni hiyo walitumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa zaidi kuhusu kile kilichotokea. “Mshambuliaji kwenye makao makuu ya YouTube. Nilisikia milio ya risasi na kuona watu wakikimbia nikiwa nimekaa katika meza yangu, ” alisema Vadim Lavrusik, meneja wa bidhaa katika kampuni hiyo. Pia alisema kuwa yeye na watu wengine walijifungia katika chumba, na baadae wakafanikiwa kutoka katika jengo hilo.


Kampuni ya Google imesema inafanya kazi kwa karibu na mamlaka na itatoa taarifa rasmi baada ya kuwa inapatikana.