Kampuni ya simu za mkononi na kompyuta Apple ilitangaza matoleo mapya ya simu mnamo Septemba 12, matoleo hayo ni pamoja na iPhone X, iPhone 8 na iPhone 8 Plus.

Katika kile kilichoonekana kuzungumzwa zaidi kuhusu matoleo hayo mapya ni jinsi kampuni ya Apple walivyoweza kubuni taswira mpya kabisa katika kioo cha simu ya iPhone X kwa kuondoa kitufe cha Nyumbani na kufunika pembe zote za uso wa simu hiyo kwa kioo. Kwa upande wa iPhone 8 na iPhone 8Plus zitaendelea kutofautishwa kwa ukubwa na kamera.

iPhone mpya
iPhone X, iPhone 8Plus na iPhone 8

Katika hayo yote kuna machache yaliyobakia kuwa mapya kwa simu zote, hakuna simu ya iPhone toleo la mwaka huu kukosa yafuatayo:

  1. Wireless charging kwa simu zote

Ingawa Samsung walifanikiwa kuleta teknolojia hii ya kuchaji simu yako bila kutumia waya wa umeme ‘USB’ mnamo 2014, na ikatumika kwenye matoleo mengi ya simu za samsung na makampuni. Apple wameamua kuleta teknolojia hiyo mwaka huu ambapo utaweza kuchaji matoleo yote mapya ya simu kwa mwaka huu bila kutumia waya, vile vile utaweza ‘eaphones’ ambazo zinatambulika kwa jina la ‘AirPod’. Jinsi ya kuchaji itakua ni kuweka simu yako juu ya kifaa chenye umbo la mviringo chenye kutambulika kwa jina ‘Qi’ chenye uwezo wa kutuma umeme kwenda kwenye simu yako bila waya.

 

iPhone X, Apple watch na AirPod juu ya chaja mpya

2. Kutoingia maji na vumbi

Jambo lingine ambalo utalikuta kwenye matoleo hayo matatu ni hili la kuweza kuzuia maji na vumbi kuingia kwenye simu yako. Bila shaka hili sio jipya, Apple waliweza kututambulisho uwezo wa kuzuia maji na vumbi kwenye simu zao kwenye toleo la mwaka jana iPhone 7. Teknolojia hiyo inakua na kipimo cha IP67. Ambacho maana yake ni kuzuia vumbi kabisa ila kutoingia maji kwa dakika 30 kwenye kina cha mita 3.3.

3. Uwezo mkubwa wa kurekodi video

Apple wemeweka uwezo wa 4K kwenye kamera za hayo matoleo, ni kipimo kikubwa katika ulimwengu wa kurekodi video. Vile vile teknolojia ‘optical image stabilization’ ya kuzuia picha au video kucheza cheza bado itapatikana kwenye matoleo ya simu zote.

Tuandikie maoni yako chini na usisahau kushare kwa wengine. Ahsante 🙂