Mara baada ya picha, sifa za Google Pixel 2 nazo zavuja

865
Pixel 2 - SwahiliBytes - swahilibytes.co.tz

Kampuni ya Google inatarajia kufanya uzinduzi wa toleo lake jipya la simu janja za Pixel ifikapo wiki ijayo, lakini tayari watu washaanza kufahamu kila kitu kuhusu toleo mpya kutokana na taarifa mbalimbali muhimu kuanza kuvuja.

Mwanzoni zilianza kuvuja picha za simu janja hizo za Pixel 2 na Pixel 2 XL na sasa zikifuatia sifa na uwezo wa simu hizo.

Soma Pia: Google yakubali kununua sehemu ya HTC kwa dola bil 1.1

Inasemekana kuwa simu hiyo ina muonekano sawa na simu ya Samsung Galaxy S8 na itakuwa na kipengele kipya kiitwacho “active edge”.

Simu janja hizo pia zitakuwa na uwezo wa kusapoti eSIM (embedded SIM card) ambapo itamuwezesha mtumiaji kuhama mitandao ya simu bila kubadilisha SIM kadi yake.

Google inatarajia kuziachia Pixel 2 ifikapo mwezi Oktoba tarehe 4.