SKYPE: Microsoft wamebadilisha muonekano wote wa programu hiyo

791

Programu ya Skype ambayo ilipata umaarufu wa kutumia mawasiliano ya uso kwa uso na unaeongea nae, wameleta mabadiliko ya muonekano kwenye simu janja na kompyuta

Microsoft wamiliki wa Skype walionyesha nia hiyo mnamo mwezi wa 8, na mabadiliko utakayokuta ni:

  • Jopo la taarifa za kuhusu Skype yako lipo karibu na urahisi wa kusoma kila kitu kwa haraka .
  • Eneo la kuona picha, file na link zote ulizosambaziana na watu kuwa karibu na rahisi kuchambua.
  • kionjo cha kutuma ‘GIF’ kutoka Giphy na kupanga tukio kwenye ‘chat’ yako.
  • Uwezo wa kuonyesha kuonyesha ishara yako ya Emoji kwenye maongezi ya uso kwa uso.
  • Utaweza kumuita mtu kwa kutumia alama ya ‘@’ kwenye kikundi cha kuchat.
  • Vile vile utapata muonekano wa usiku “Night Mode” ili usipate shida ya kuona vizuri kutokana na mwanga mkali.
  • Kama ilivyo mitandao mikubwa ya kijamii (Instagram, Facebook, Snapchat, WhatsApp) imepewa ‘Story-feature’ basi pia utakuta kionjo hiki pale ukianza kutumia programu ya Skype.

Soma pia:

Haya yote utaweza kuyapata kama Kompyuta yako inapakua ‘updates’ bila kuhitaji ruhusa, au tembelea tovuti ya Skype kupakua programu hiyo kwa mtumiaji wa Windows, Mac, Linux, Simu janja, Xbox na Saa janja.