Snapchat yapanga kuzindua michezo katika programu yake

141
snapchat logo

Kampuni ya teknolojia na kamera Snap Inc. imetajwa kuzindua michezo (games) katika programu yake maarufu ya Snapchat, The Information imeripoti.

Kulingana na ripoti, Snap tayari ishaanza kusaini mikataba na wachapishaji mbalimbali wa michezo, inapanga kuanza kutoa huduma hiyo kwa watumiaji wake hapo baadae mwaka huu.

Snap pia itawaruhusu watengenezaji wengine wa michezo kutengeneza michezo itakayoweza kuchezwa katika programu yake ili kuwafanya watumiaji wake kutumia muda mwingi zaidi katika programu hiyo.

SOMA PIA: Kampuni ya Bakhresa kuja na mtandao wa Azam Telecom

Kuongezwa kwa michezo katika programu hiyo kutawezesha kuongezeka kwa mapato kupitia matangazo na pia itajiongezea watumiaji wapya wengi zaidi.

Snapchat haitokuwa programu ya kwanza ya mitandao ya kijamii kupanua wigo wa kimtandao na kuongeza michezo ili kuwaburudisha watumiaji wake, WeChat nayo wamefanya hivyo pia mapema mwaka huu.