Snapchat yenye muonekano mpya inawapa watu wengi hasira

797
Snapchat mpya

Programu ya Snapchat iliyo na umaarufu kwa vijana, imebadilisha muonekano wake wa programu nzima na kuwaacha watumiaji wakipata hasira, imezidi kuwa ngumu kutumia

‘Stories’ sasa zinapatikana kwa upande wa kulia, ambazo zamani zilipatikana upande wa kushoto. Huo upande wa kulia umejaa video za watu maaraufu duniani na video kutoka kwenye kampuni za burudani na magazeti.  ‘Stories’ zako utazipata kwenye profile yako, au kwa kubofya ‘Bitmoji’ kwa upande wa marafiki kwa juu.

Pia sasa utaona marafiki unayowasiliana nao kwa sana wanakuja na stories zao kwenye orodha ya marafiki wako wote.

Snapchat mpya

 

Soma Pia: Samsung ipo karibuni kuzindua Galaxy S9

Watumiaji wa Snapchat, wametumia mtandao wa Twitter kuonyesha hisia zao za kutoipenda.