SpaceX imefanikiwa kurusha roketi kubwa iliyobeba gari kwenda angani

815
Gari ndani ya roketi

Roketi ya Falcon Heavy ilirusha hapo jana, kutoka kwenye eneo ambalo NASA ilikua ikituma kurusha roketi kwenda mwezini zaidi ya miaka 40 iliyopita

Elon Musk CEO wa SpaceX ambae pia anamiliki magari ya umeme ya Tesla, aliamua kuweka gari moja aina ya Tesla Roadster kwenye roketi moja ambayo ilielekezwa kwenye sayari ya Mars. Kwa kutumia mitandao ya kijamii Elon Musk alisema gari hilo linaweza kufika karibu na sayari hiyo baada ya miezi sita kuanzia sasa.

Soma Pia: China yatuhumiwa kufanya udukuzi kwa Umoja wa Afrika

Safari hii ya roketi ni moja majaribio na kujifunza zaidi ili mpango  wa SpaceX kupeleka watu kwenye sayari ya Mars uje kufanikiwa. Kupitia Twitter Raisi wa marekani Donald Trump alimpa pongezi Elon Musk kwa mafanikio ya kurusha roketi mbili.

 

Tuachie maoni yako hapo chini!