Swahili imekua lugha ya kwanza Afrika kutambulika kwenye Twitter

210

Kwa muda mrefu sana kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ulikua unaonyesha utambuzi wa lugha za afrika kwa kusema ni za Indonesia katika kuzitafsiri.

Sasa hilo limebadilika kwa Twitter kuitambua lugha ya Kiswahili na kuipa uwezo kwa kutafsiri kutoka lugha mbalimbali kubwa duniani.

Swahili imekua lugha kubwa na kutumiwa kwa wingi kwenye nchi za afrika mashariki pamoja na sehemu mbali mbali duniani. Ni lugha ya 15 kwa watumiaji wengi, takribani watu milioni 98.8 wanatumia lugha hiyo.

Soma Pia:Facebook yafuta akaunti feki milioni 583 katika kipindi cha miezi mitatu

Utambuzi huo haukuja hivi hivi, ni kutokana na juhudi za watumiaji wa Twitter kuanzisha Hashtag za #SwahiliIsNotIndonesian and #TwitterRecognizeSwahili na kuendelea kuwakumbusha makao makuu ya Twitter kuwa wanakosea kwa kutoitambua Swahili.