TAFITI: Asimilia 80 ya vijana wanapendelea iPhone kuliko Android

667

Uthamani wa brand (brand value) ya Apple, kampuni kubwa ya teknolojia iko mbali zaidi ya simu nyingine yoyote ya Android, na hiyo inashuhudiwa kutokana na mauzo makubwa ambayo iPhone hupata mwaka baada ya mwaka, licha ya ongezeko la bei.

Kulingana na tafiti ya Piper Jaffray kwa vijana wa Amerika wenye wastani wa umri wa miaka 16, 82% ya walioshiriki zoezi hilo wanapendelea iPhone kuliko Android. Hii ni asilimia kubwa zaidi katika historia ya tafiti zilizowahi kufanywa na kampuni hii, ambayo inaonesha wazi kuwa umaarufu wa simu za iPhone kutoka Apple ni mkubwa sana.

Umaarufu huu unaonekana kuwa utaongezeka maradufu, kutokana na kwamba kati ya washiriki hawa wamehakikishia kuwa 84% ya wao watanunua iPhone nyingine kama simu yao inayofuata.

SOMA PIA: Apple yainunua Shazam kwa dola milioni 400

Uchambuzi wa Piper Jaffray unaamini kwamba kampuni ya Apple itazindua iPhone mpya tatu baadaye mwaka huu, na umaarufu wake utaendelea kukua ingawa kwamba ni kweli moja ya simu hizo zinaweza kuzidi $1100 (TZS 2,500,000), pia kampuni ya Apple itazindua simu ya nafuu ambayo itakua ndani ya uwezo wa vijana hao.

iphone-tafiti-graph

Kama inavyoonekana katika grafu inayoambatana na habari hii, katika miaka minne iliyopita kumekua na ongezeko kwa zaidi ya 20% ya wamiliki wa simu za iPhone, ambayo inaonesha kuwa pamoja na usambazaji mzuri wa bidhaa za Android, vijana wa Amerika wanaendelea kupendelea bidhaa za kampuni ya Apple.

Tafiti hizi zimefanyika nchini Marekani pekee, zinaweza kuwa na mabadiliko sehemu zingine duniani, Tuambie maoni yako hapo chini. Unaweza kushare pia kwa rafiki zako.