Tanzania imeleta sheria na taratibu kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii

1096
Tanzania na mitandao ya kijamii

Tanzania wameingia kwenye sheria mpya ya utaratibu wa kuendesha mitandao ya kijamii na blogu, Utaratibu huo ulipendekezwa na TCRA mnamo mwaka 2017, na kufikia hatma ya kuanza kutumika mwaka huu 2018

katika vipengele vyenye kuvutia hoja mbali mbali ni serikali kutaka malipo kwa wote wanaoendesha redio za internet na kuweka video kwenye tovuti.

Wanaoendesha blogu watatakiwa kuomba leseni kutoka TCRA, na kulipia ada ya mwaka baada ya kupata leseni, kama ilivyo kwa redio za mitandaoni na tovuti.

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe amethibitisha hilo kwa kuweka sahihi katika sheria hiyo.

Serikali ya Tanzania imesema utaratibu huo utasaidia kuzuia uovu wa maadili unaosababishwa na mitandao ya kijamii na intaneti kwa ujumla, na kuongeza usalama wa taifa zima.

Pia katika utaratibu huo kuna kipengele cha kuwataka watanzania wote kuweka password (PIN) kwenye simu zao, na kama kusema uvunjwaji wa sheria hii utapigwa faini ya takribani milioni 5 au kufungwa jela miezi 12 au vyote kulingana na mahakama itakavyoamua.

Soma Pia: Facebook yapata kashfa nzito kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya

Wanaoweka video, blogu, nakala na podcast watalipa TSHS 100,000 kuomba leseni, na gharama ya mwanzo kwenye leseni TSHS 1,000,000 na ada ya mwaka TSHS 1,000,000. Hii inamaana kuendesha blogu ndogo ya kwako itakugharimu kufikia TSHS 2,000,000 na zaidi katika leseni.

Soma Pia: TTCL yazindua huduma mpya ya internet kwa matumizi ya nyumbani

Bila wasiwasi sheria hii inapinga haki za msingi kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii na intaneti kwa ujumla. Tuachie maoni yako kwenye comment chini.

Ongea na sisi kwenye Twitter, tutakujibu!