Tigo yaungana na Selcom na Mastercard kuleta huduma ya Mastercard QR Tanzania

872
tigo-mastercard-qr

Kampuni ya simu nchini Tanzania Tigo, Selcom na Mastercard waungana kuleta huduma ya Masterpass Quick Response (QR) nchini Tanzania kupitia Tigo Pesa.

Ifikapo mwezi wa nne mwaka huu, takribani milioni saba ya watumiaji wa huduma ya Tigo Pesa watanufaika na huduma hiyo ili kuweza kufanya manunuzi mbalimbali kwa kuscan QR code katika app ya Tigo Pesa.

Huduma hiyo pia haitowakosa watumiaji wa simu za kawaida kwani nao wamewezeshwa kutumia menyu ya USSD na kisha kuandika code ya kipekee ya muuzaji ambayo itakuwa chini ya QR code.

SOMA PIA: Microsoft kumpa vifaa mwalimu wa Ghana anaefundisha kompyuta ubaoni

Simon Karikari, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania alisema Tigo Pesa sio tu ni huduma ya kuweka na kutoa fedha, bali ni mfumo unaowezesha wateja kupata huduma mbalimbali za kifedha akaongeza Masterpass QR ni ongezeko jipya katika huduma zinazotolewa na TigoPesa ili kuendelea kuwarahisishia wateja katika maisha yao ya kila siku.

Raisi wa Mastercard tawi la Sub-Saharan Africa bwana Raghav Prasad amesema muungano huu ni hatua moja kubwa katika kuboresha usalama kwa wateja linapokuja swala la miamala. Akafanunua zaidi kuwa Afrika karibu asilimia 85 ya manunuzi ya rejareja yanafanyika kwa cash, mfumo salama na unaopatikana kiurahisi ndio jibu sahihi juu ya tatizo hilo.