Toleo la FIFA18 limewadia, na haya ndo mapya yake

957
Fifa 18 kwenye PS4 na Xbox One
Fifa 18 kwenye PS4 na Xbox One

Kila mwaka imekua ni utamaduni wa matoleo ya fifa kutoka, mwaka huu FIFA 18 ikiwa na picha Cristiano Ronaldo kwenye mfuniko kwa mara ya kwanza katika historia

Tarehe za matoleo ya Fifa 18

Ina tarehe aina tatu za matoleo yake, ambayo yana njia na sababu tofauti.

Septemba 21 – Wachezaji (gamers) wote wenye ‘EA access’ ndo wakwanza kuipata

Septemba 26 – Wachezaji (gamers)wote wanaofanya ununuzi wa awali.

Septemba 29 – Toleo la dunia nzima kwa wote kuachiwa kila sehemu.

Aina za fifa 18

  1. Kutakua na Fifa 18 ya kuchezwa kwenye ‘console’ ya PS4(Playstation 4) na kaka yake PS4 Pro, na kwa upande mwingine. inakuwepo ya Xbox One ambayo inachezwa pia kwenye Xbox Scorpio.
  2. Kwa upande wa Xbox 360 na PS3 ambazo ni ‘console’ za zamani, zinapewa Fifa 18 Legacy ambayo haina ‘The Journey’ kuanzia toleo za Fifa 17 na Fifa 18.
  3. ‘console’ ya Nintendo switch imepewa ila bila kutumia jina la ‘Fifa 18’ na kubadilishwa baadhi ya vitu kwenye mchezo huo wa mpira.

Nini kipya kwenye Fifa 18?

Mfuniko wa Fifa 18
Mfuniko wa Fifa 18

Kama ilivyo kawaida ya matoleo mapya, huwa na muonekano, chenga na uhalisia kuongezeka kuliko toleo la nyuma yake. Haya ndo mabadiliko utakayo yaona ukicheza Fifa mpya;

‘Graphics’

Kwa mara ya pili itatumia teknolojia ya ‘frostbite’ kuonyesha muonekano wa mchezo mzima. Miale ya mwanga na vivuli kuanzia kwenye uwanja, washabiki hadi kwa wachezaji kuonekana kwa mvuto zaidi.

‘Animation’

Katika malamiko makubwa Fifa wamekua wakipata ya hapa na pale ni michezo kuganda ganda ‘laggy’ na mchezaji kuchelewa kufanya unachotarajia, kwa mwaka huu mfumo nzima wa ‘animation’ umetengenezwa upya, na kila mchezaji wa mpira kwenye ‘Fifa 18’ anafanya kama alivyo kwenye ukweli uwanjani.

Viwanja

Viwanja vimeongezewa uhalisia, kama kiwanja kina hali ngumu ya kucheza na kwenye Fifa 18 kutakua na hali hiyo hiyo.

Jua njia rahisi ya kupunguza faili nyingi kwenye kompyuta iliyojaa

Washabiki

Washabiki wameongezewa ukweli zaidi kwa kutumia teknolojia ya ‘AI’ kwenye muonekano na ushangiliaji wa magoli, ingawa bado kuna mrudio wa ushangiliaji.

Wachezaji

Wachezaji wenye majina makubwa duniani wameongezewa uhalisia wao kama ilivyo ukweli, na animation za kwao peke yao.

Uchocheaji wa mpira

Uwezo wa ‘dribbling’ umeshuhudiwa kuwa na uhalisia zaidi kuliko vinginevyo, na kwenye Fifa 18 utapata marekebisho na ugumu mwingine wa kuendesha mchezaji akiwa na mpira.

‘Artificial Intelligence’

Pasi za wachezaji zitakua zinaenda kutokana na uwezo kila mchezaji kwenye timu, pia na kufanya maamuzi ya akili zaidi kulingana na uhalisia wake.

Kubadilisha wachezaji

Kwa sasa sio lazima kusimamisha mchezo ili ubadilishe wachezaji, wakati mechi inaendelea kuna sehemu upande wa kulia ni kubofya na pale mpira utakapo simama labda kutoka nje mabadiliko ya wachezaji yatafanyika. Utakua unapanga nani wakuingia na wakutoka kabla mechi haijaanza au Fifa 18 itakusaidia kuchagua.

Magoli

Majaribio ya magoli yameongezewa urahisi wa kufunga tofauti na Fifa 17 ambayo ni rahisi kwa wazuiaji wa timu kukunyang’anya mpira, vile vile magoli ya ‘volley’ ni rahisi kufunga ingawa bado uwezekano wa kupaisha juu upo pale pale.

Ukabaji

Pale uwezo wa kushinda ulipo ongezewa na wazuiaji wamepewa uwezo zaidi kuleta ugumu kwenye mchezo huo.

‘The Journey’ na mbinu za timu ni mengineyo yaliyopewa mabadiliko katika toleo la fifa 18.

Angalia ‘trailer’ hapo chini

Usisite kutoa maoni yako na kushare kwa marafiki, pia comment hapo chini kama ukitaka kucheza na wanaojua ili upime kiwango chako cha Fifa 17 kabla hujahamia toleo jipya la Fifa 18

Google yakubali kununua sehemu ya HTC kwa dola bil 1.1