TTCL yazindua huduma mpya ya internet kwa matumizi ya nyumbani

925

Kampuni ya mawasiliano ya TTCL Corporation imezindua huduma yake mpya iliyopewa jina la Fiber Connect Bundle. Huduma hii mpya itamuwezesha mteja kupata huduma nnne kwa pamoja zikiwa na unafuu mkubwa wa gharama na ubora wa hali ya juu.

Kupitia kifurushi cha Fiber Connect, Mteja ataweza kufaidika na huduma zifuatazo;
Kwanza, Mteja atapata Intaneti yenye kasi isiyo na kikomo( Unlimited).

Pili, Mteja atapata huduma ya simu za sauti kwa simu za mezani na (Sim Card) ambayo ataitumia kwenye simu yake ya mkononi na kupata huduma ya Intaneti sawa na simu ile anayopata katika simu ya mezani.

Soma pia: Vivo yawapiku Apple na Samsung, teknolojia ya fingerprint

Huduma ya tatu , Mteja atapata huduma za wireless service (WiFi) katika nyumba yake ambapo vifaa vyote vinavyotumia Teknolojia ya Intaneti vitaunganishwa na kuweza kutumia huduma hii. Mfano wa vifaa husika ni Smart Tv, Tablets, Laptops na kadhalika.

Nne, Mteja atapatiwa vifaa vyote bure pamoja na uhakika wa huduma za baada (After Sells Services) endapo itahitajika.

Mradi huu unatarajiwa kufikisha huduma katika nyumba zipatazo 500 katika eneo la Mikocheni, Nyumba 500 zingine katika eneo la Mbezi Beach na nyumba zaidi ya 200 katika eneo la Medeli Mkoani DODOMA.