Twitter imetambulisha kipengele kipya cha kuhifadhi tweets

694

Katika hali ya kuendelea kutoa njia mbadala kwa watumiaji wake zitakazowawezesha kuongeza ufanisi wa utumiaji wa mtandao huo, sasa developers wa Twitter wameanza kufanya majaribio ya kipengele kipya kitachomuwezesha mtumiaji kuhifadhi tweets au machapisho ili aweze kuzisoma baadae.

 

Twitter imeunda kipengele kipya cha kuhifadhi tweets ili uweze kuzisoma baadae

Kama kuna kitu hatuwezi kukataa ni kua Twitter pamoja na mameneja wake kila siku wanatafuta njia mbadala ili watumiaji wao waaminifu waweze kuendelea kutumia, na kuongeza ufanisi ya utumiaji wao wa mtandao wao na kuzidi kuutumia kadri ya muda unavyozidi kwenda.

Soma Pia: Hyatt: Shirika kubwa la hoteli duniani limeibiwa data za malipo(Visa card & Mastercard) na wadukuzu

Kwa mfano kwenye kipindi cha miezi kadhaa iliyopita tumeona jinsi walivyobadilisha kabisa muonekano wa mtandao wao kwenye vifaa vyote (simu janja na kompyuta) na siku chache zilizopita baadhi ya watumiaji wamepata uwezekano wa kuongeza herufi mpaka kufikia herufi 280, na kupanua kikomo kilichowekwa toka kuanzilishwa kwa mtandao huo.

Na sasa tunapata habari mtandao huo wa kijamii, Twitter sasa unaendeleza kipengele kitakachowezesha kuhifadhi machapisho au tweets ili ziweze kusomeka baadae.

Taarifa zimeibuka kutoka kwa Jesar Shah, Meneja wa Bidhaa kutoka Twitter ambaye ameonesha kipengele hicho kichachoonesha mfumo wa awali (prototype) baada ya wiki moja ya majaribio.

 

Kama unavyoweza kuona kila “tweet” ina menyu kwa chini ambayo inajumuisha chaguo ‘Add to bookmarks’, orodha kamili ya machapisho/tweets zilizohifadhiwa inaweza kutizamwa kwenye profile ya mtumiaji.

Vile vile Shah amewaeleza wafuasi wake kueneza alama ya #SaveForLater, ili watumiaji wengine waweze kutoa mapendekezo ya kuboresha kipengele hicho kipya.

Bila shaka kipengele hiki kipya kitawasaidia watumiaji wengi wa mtandao huo wa kijamii kuhifadhi machapisho/tweets ambayo wanayaona kuwa muhimu na kuhifadhi kwa kusoma baadae.

So, unafikiria nini kuhusu hili? Unaweza kutuachia maoni yako katika hili hapo chini.