Twitter yaongeza mara mbili kiwango cha maneno katika tweet

842
Twittter - SwahiliBytes - swahilibytes.co.tz

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 11, kampuni ya Twitter imeongeza kiwango cha maneno katika tweet ambapo awali kilikuwa ni 140.

Kampuni hiyo ilitangaza hapo Jumanne kuwa itaanza kufanya jaribio la kiwango kipya cha maneno ambayo ni 280 kwa lugha zote kasoro Kijapani, Kichina na Kikorea.

Soma Pia: WhatsApp imezuiwa matumizi nchini China, orodha ya mitandao ni zaidi ya 3,000 imezuiwa hadi sasa

Kampuni pia imeeleza kuwa sababu ya kutoongeza kiwango cha maneno kwa lugha hizo ni kuwa lugha hizo kutoka barani Asia zinajitosheleza kutoa ujumbe mara mbili zaidi katika herufi moja ukilinganisha na lugha nyingine.

Hoja hiyo ya kuongeza kiwango cha maneno itawapa uhuru zaidi watumiaji wa Twitter kujielezea katika mtandao huo kuliko hapo mwanzo wakati mtumiaji alipaswa kubana maneno ili kuweza kutosha idadi ya maneno 140.

1 COMMENT

Comments are closed.