Twitter yatambulisha herufi 280 kwa watumiaji wote

862

Baada ya kufanya majaribio kwa miezi kadhaa, Twitter imeanza kuachia kipengele kipya kinachomuwezesha mtumiaji kutumia herufi 280 tofauti na herufi 140 ambazo ilikua ikiruhusu hapo awali , kuanzia leo.

Twitter imesema tusitegemee kuona mafuriko ya matumizi mabaya ya kipengele hiki. Kutokana na data walizokusanya kipindi cha majaribio ya kipengele hiki, idadi ya tweets zilizokua na urefu zaidi ya kawaida ilikua ndogo sana. Ni asilimia 5 (5%) ya tweets zilizotumwa na waliokua wakifanya majaribio ndizo zilikua na urefu wa herufi zaidi ya 140.
Unaweza kupata kipengele hiki kipya katika toleo jipya la programu ya Twitter katika vifaa vyote (iOs, Android na Desktop)
herufi 280
Kipengele hiki kipya kitapatikana katika lugha zote zenye matatizo ya kua na maneno marefu, Kwa mujibu wa msemaji wa Twitter, lugha za Kijapani, Kikorea, na Kichina hazihitaji kikomo kikubwa cha herufi kutokana na lugha hizi kuwa na asili ya herufi moja kuwa na uwezo wa kubeba ujumbe mrefu.