Uber: Wadukuzi wamehack na kuiba data za watumiaji milioni 57

1361

Uber wamelipa kiasi cha $100,000 kwa wadukuzi hao ili wafute hizo data walizoiba na wakae kimya, pia imefukuza afisa usalama Joe Sullivan na viongozi wengine wa juu kutokana na tukio hilo

Data  zilizoibiwa ni kuanzia mwaka 2016 za majina, barua pepe na namba za simu, leseni takribani 600,000. Uber wamesema wadukuzi hawajaiba data za kadi ya Visa/Mastercard, historia ya safari, na zinginezo.

Jinsi walivyoibiwa na wadukuzi hao wawili ni baada ya mtaalamu wao kuibiwa ‘password’ ya mtandao wa Github ambao wataalamu wa kutengeza programu hupendelea kuutumia. Wakafanikiwa kuingia mahali ambapo Uber wanatunza data hizo (Amazon Web Services), baada ya kuiba wakawatumia Uber barua pepe ya kuwaomba hela.

Soma pia: UBER: Waonyesha jinsi helikopta-taxi zao za UberAir zitakavyofanya kazi

Uber wamesema walichukua hatua muhimu za kuongeza usalama zaidi kuzuia jambo hilo la udukuzi kutokea tena.