UBER: Waonyesha jinsi helikopta-taxi zao za UberAir zitakavyofanya kazi

743

Uber kampuni ya kuhudumia kwa usafiri wa magari kwa mtindo wa Taxi, imefanya mkutano wake huko Lisbon na kuonyesha jinsi helikopta-taxi itakavyofanya kazi

Uber walionyesha mipango ya kufanya huduma hiyo tangu mwaka 2016 na kusema itaitwa UberAIR

UberAir ni ndege ndogo ya umeme ambayo itanyanyuka kwenda juu kama helikopta, huduma hii itasaidia kuokoa muda wako kwa bei ndogo. Uber wanashirikiana na NASA, Aurora Flight Sciences, Pipistrel Aircraft, Embraer, Mooney na Bell Helicopter.

Pia kampuni ya ChargePoint itahusika kutengeneza vifaa na mfumo mzima wa kuweka umeme, maana haitatumia mafuta kama ndege nyingine ili kutoharibu mazingira. Huduma hiyo imepangwa kuanza ifikapo mwaka 2020.

Soma Pia: Elon Musk aonyesha mpango wa huduma za usafiri wa chini ya dakika 30 kwa roketi