Samsung nayo yarushiwa vijembe na Huawei katika tangazo lao

1504
Wote tunafahamu vita kali ya makampuni ya kutengeneza simu ili kuweza kua na wateja wengi duniani haitokuja kuisha.

 

Na kama tunavyotambua Huawei na Samsung ni moja ya makampuni makubwa duniani, hii inafanya kila kampuni kuangalia mikakati bora ya kutangaza bidhaa zake. Hivyo hivi karibuni, Huawei wametengeneza video ya kuidhihaki kampuni ya Samsung.

 

 

Wiki kadhaa zilizopita Huawei walitangaza simu yao mpya aina ya Mate 10. Simu hii ilikuja na sifa zote za kujiweka kama moja ya simu janja bora zaidi kwa mwisho wa mwaka 2017 na mwanzo wa mwaka 2018.

 

Battery yake yenye uwezo wa 4,000 mAh inashindana na simu nyingine zenye uwezo wa juu (high-end). Hivyo ndivyo kampuni yake inajua, ndio maana imeamua kuja na mkakati huu wa kuitangaza.

 

 

Ukitazama sekunde 15 za video hiyo, katika maudhui sawa utaona scene 5 zenye ujumbe ulio wazi: kwamba Huawei Mate 10 ina uhuru zaidi kuliko Samsung Galaxy S8.

 

Ingawa hakuna sehemu katika video hiyo inayoashiria wazi ni dongo la Samsung moja kwa moja, lakini ukiangalia nyuma ya simu hizo, inathibitisha ushindani kati ya kampuni hizo mbili.