Vinjari kwa simu janja yako bila matangazo yanayokera (Ads)

881

Ukutumia Intaneti, simu Janja au kwa komputa taarifa zako nyingi zinachukuliwa na makampuni yanayotengeneza hivyo vitu(simu, saa, tv janja, kivinjari)

Kwa mfano ukitembelea YouTube ukaona tangazo la gari, au tangazo la kazi hiyo ni kwa sababu ushatembelea mitandao ya kazi au ulishatafuta kazi kwenye tovuti ya google sasa wametunza taarifa zako na kujua unataka nini, kisha kukutumia tangazo kutokana na taarifa walizozitunza, baadhi ya taarifa zinazotunzwa ni;

Vitu unavyofanya

 • Vitu unavyotafuta (Google Search)
 • Tovuti unazotembelea
 • Video unazoangalia
 • Matangazo unayobonyeza
 • Sehemu ulipo(location)
 • Maelezo ya kifaa (OS, Apps)
 • anuani ya mtandao wako (IP address) na cookie data

Vitu unavyotengeneza

 • Barua pepe
 • Tukio la kwenye kalenda ya simu janja yako yako
 • Picha za mnato na video unazoangalia

Kampuni ya Firerox imekuletea kivinjari cha Focus ambacho kimetengenezwa kwa ajili ya ulinzi wa taarifa zako na pia uwe na faraga unapotumia intaneti. Kwa urahisi futa historia ya vitu ulivyofanya au kutafuta, cookie, Nywila, bookmarks na kuepusha matangazo ambayo huyapendi.

Soma Pia: Njia rahisi ya kupunguza faili nyingi kwenye kompyuta iliyojaa

Jinsi ya kutumia Firefox Focus

 1. Kama unataka faragha na hautaki kufatiliwa, ingia Google Play au App Store na upakue Firefox Focus

2. Futa taarifa zako zote kwa kipindi ulichokua unatumia internet kwa urahisi kwa kubofya kitufe ya Erase kwenye sehemu ya ‘search’.

Tumia Mozila Focus na Kivinjari cha safari kwa wenye simu za iPhone

 1. Bonyeza Settings kwenye iPhone or iPad.
 2. Shuka hadi kwenye Safari, kisha ibonyeze.

3. Bonyeza Content Blockers.

 

4. Kisha baada ya Firefox button kiwashe

Kuwezesha Focus kwenye safari.

 1. Nenda kwenye application ya Focus Kisha bonyeza ikoni (icon) kama ya gia kwenye upande wa kulia juu.
 2. Baada ya hapo bonyeza switch kwenye Safari kuiwezesha kufanya kazi

Pia unaweza kubadilisha vitu kama

kuna njia nyingi za kuvinjari kwa faraga kwa kutumia vitu kama vpn, incognito mode kwenye kivinjari cha google chrome, private mode kwenye kivinjari  cha mozila.

kama una maswali au unataka wataalamu wetu wakusaidie, unaweza kutuachia maoni yako katika hili hapo chini