Vipengele 10 vya muhimu kwenye iOS 12 inayokuja hivi karibuni

150

Kama ilivyo tamaduni ya Apple kila mwaka kuleta matoleo mapya ya simu za iPhone, kompyuta mpya za Macbook na iMac. Mwaka huu wametangaza vipengele 10 vya mabadiliko ya iOS ambayo ni progamu kiendeshi ya simu za iPhone na iPad zote.

1. Ufanisi bora zaidi

Apple waliweka wazi kwamba iOS 12 imepewa kipaumbele kwenye ufanisi wake na ufanyaji kazi ziadi kwenye programu kiendeshi(Operating System). spidi ya kufungua programu za simu imeongezeka kwa asilimia 40%, asilimia 70% kwenye ufunguaji wa kamera kutoka kwenye lockscreen na asilimia 50% kwenye utumiaji wa keyboard katika kuandika na mengineyo.

2.  Screen Time

Apple wamesema wanataka simu iwe na mahusiano ya mazuri na watumiaji, kwa kuongeza kipengele cha Screen Time kinachokupa uwezo wa kuangalia ni jinsi gani unavyotumia muda wako na programu zote, na kukupa maelezo ya wapi utapoteza muda mwingi. Vile vile kukupa uwezo wa kufatilia utumiaji wa simu za watoto wako, na kupewa repoti ya matumizi yote kila wiki.

3. Memoji

iOS 12 itakupa uwezo wa kutengeneza Emoji ya kulingana ulivyo, kuchagua rangi, nywele, nguo na zaidi. Pia itaweza kutambua ukiwa unatoa ulimi nje au kukonyeza kwa macho yako na alama za sura zote, na kutumia kwenye FaceTime.

4.Notifications

Sasa notifications zitakua kwenye vikundi, kulingana na mada inayozungumziwa. Hii itakurahisishia kujua kwa ujumla bila kusoma notification moja moja.

5 Siri Shortcuts

Sasa programu ya usaidizi ya Siri itakupa uwezo wa kutengeneza njia mkato za vitu unavyotaka kufanya. Kwa mfano utaweza kuaambia familia yako upo njiani kwenda nyumbani, na huo ujumbe utawasha taa kupitia programu ya HomeKit na pia itakuleta ramani, hayo yote utayapata kwa kuiambia Siri “I’m going home”. Hizo sheria zote utatengeneza wewe na kuongea kupita iPad, Apple Watch, iPhone au HomePod.

6. Group FaceTime

FaceTime itaongezewa uwezo wa kuongea na watu 32 kwa pamoja, na kwa iOS na macOS. Mtu akiwa anaongea kioo chake cha FaceTime kitakua kikubwa kuliko wote ili wote wasikilize.

7. ARKit

Kipengele hiki kita husu wanatengeneza programu za iPhone, waweze kuongeza ujuzi na maujanja kwenye teknolojia ya AR( Augmented Reality). Sasa ARKit itaweza kutambua vitu kwa kamera ya simu na kuleta hizo data kwenye utumiaji bora wa mwenye simu.

8. Measure App

Katika kipengele cha ARKit, Apple wameleta Measure App. Utaweza kupima urefu wa vitu vyenye umbo la mstatili kama meza, na kupata vipimo vyake vya urefu na upana. Itakupa uwezo wa kupima kama kifaa cha Tape measure ya fundi ujenzi.

9. Camera

Apple wameongeza ubora kwenye Camera ya iOS 12. Mwanga wa kutosha kwenye simu zenye ‘Potrait Mode’, QR codes zitakua rahisi kusoma ziadi ya ilivyo kwenye iOS 11

 Soma Pia: Vivo: Simu ya kwanza duniani kusoma alama za vidole kwenye kioo

10. Photos

Sasa utakuta sehemu maalumu kwa ajili ya picha zenye ubora zaidi, kipengele cha ‘effects’ na cha ‘sharing suggestions’. Apple watakusaidia kuchagua picha bora na watu waliopo ili iwe rahisi kama umepiga picha nyingi. Na kukushauri ‘effects’ za kutumia kwa kila picha.

Ongea na mimi kwenye Twitter.