Vivinjari 5 bora mmbadala wa Firefox na Chrome kwa mwaka 2018

221
vinjari vitano

Sisi sote tunajua kwamba kivinjari(browser) ni moja ya programu muhimu zaidi ambayo unahitaji kwenye PC yako. Kwa hiyo, leo tutawasilisha orodha ya vivinjari vitano (5) bora ambavyo unapaswa kujaribu mwaka 2018 kama mmbadala wa vivinjari maarufu zaidi duniani, Firefox na Google Chrome, kwa kuzingatia vipengele vinavyotoa kila kivinjari.

1. Opera Neon
Kivinjari cha kwanza ni Opera Neon, kivinjari hiki kimepata mafanikio ya kupata watumiaji kwa haraka kutokana na uzuri wake na ukisasa. Katika kivinjari hiki, vichupo (tabs) hazitakuwepo tena, seti za icons zitakua kama mmbadala. Utafutaji pia unafanywa moja kwa moja kutoka kwa mazingira ya kivinjari.

2. Vivaldi
Ilipewa jina baada ya Vivaldi, kivinjari hiki kiliundwa na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani na mwanzilishi wa Opera Software, Jon von Tetzchner (ambaye alitoka Opera mwaka 2011) na kivinjari hiki kina vipengele kadhaa vya kusisimua vinavyohusishwa na teknolojia za kisasa.

3. MxNitro
MxNitro, Maxton ni mojawapo ya vivinjari vya mtandao chenye kasi zaidi. Sio tu ya haraka kufungua na kuwasilisha kurasa za wavuti, lakini pia ni ya haraka sana kuifungua na kuanza kutumia.

4. Torch
Torch ni moja ya kivinjari maarufu kwenye mtandao. Kivinjari hiki kinakuja na media player, Media Grabber, (inayokuwezesha kushusha video na sauti kwa urahisi), michezo, uwezo wa kupakua torrent moja kwa moja.

5. UC Browser
UC Browser kwa kompyuta inaruhusu watumiaji kufurahia kuvinjari tovuti na matumizi ya chini ya data. In kipengele cha usalama kipya kinachohakikisha usafirishaji salama kwa kuzuia vyanzo vya programu zisizo salama (malware) na virusi kabla ya kupata fursa ya kuingia kwenye kompyuta yako. Kivinjari hiki pia kina kipengele cha kuzuia matangazo ndani yake.

Orodha hii ni baadhi ya vivinjari unavyoweza kutumia kama mmbadala wa Firefox na Google Chrome, ingawa kuna vingine vingi zaidi.

SOMA PIA: Microsoft Edge kuja na kizuia matangazo kwenye iOS na Android

Ni kipi kati ya vivinjari umeshawahi kutumi?. Tuachie maoni yako hapo chini.