Vivo: Simu ya kwanza duniani kusoma alama za vidole kwenye kioo

312

Kwa miaka mingi kumekua na tetesi kati ya kampuni kubwa za simu Samsung na Apple kujaribu teknolojia ya kusoma alama za vidole kwenye kioo cha simu.

Sasa kampuni tofauti na hizo imefanikiwa kuleta teknolojia hiyo. Vivo ni kampuni ya simu inayomiliki matoleo ya simu kama Oppo na OnePlus, imetangaza simu hiyo hivi karibuni.

Hitaji la simu kuwa na teknolojia ya kusoma alama za vidole kwenye kioo limeongezeka, lakini kampuni kubwa Google, Samsung wameishia kuweka kwa nyuma ya simu na sio kwenye kioo. Apple nao wakatoa iPhone X ambayo ipo tofauti, haina teknolojia ya alama za vidole bali inasoma sura na kutambua sura ya mmiliki wa simu.

 

Vivo X20 Plus UD ni simu pekee kwa sasa yenye teknolojia hiyo, huku ikiwa na ukubwa wa inchi 6.43 na kioo chenye uwiano wa 2160 X 1080, kamera mbili zenye 12MP na betri ya ujazo wa 3,905mAh

Soma Pia:

1. TAFITI: Asimilia 80 ya vijana wanapendelea iPhone kuliko Android 

2. VAR: Fahamu kuhusu mfumo mpya wa FIFA unaotumika Kombe la Dunia

Angalia video chini, ikionyesha jinsi simu hiyo inavyofanya kazi

Ongea na mimi kwenye Twitter, nitakujibu!