Vivo yawapiku Apple na Samsung, teknolojia ya fingerprint

809

Baada ya uvumi wa mwaka mzima kuhusu kama kampuni za Apple ama Samsung wanaweza kuweka sensor ya vidole(fingerprint) chini ya kioo cha simu zao maarufu, kampuni ya Vivo kutoka China imewapiku na kua ya kwanza kufanikisha hilo.

Katika kongamano la CES 2018, Vivo walionesha smartphone ya kwanza iliyo na teknolojia hii ya kisasa iliyopo ndani ya moja ya simu zake.

Soma pia: Snapchat yenye muonekano mpya inawapa watu wengi hasira

Kampuni ya Vivo imeungana na Synaptics, kampuni maarufu ya kutengeneza touch skrini na mouse za laptop kutoka Marekani kuwezesha teknolojia hii kufanikiwa. Vivo wanatumia sensor mpya ya Synaptics Optical sensor, ambayo imekuwa ikitengenezwa kwa miaka kadhaa.

Synaptics Optical sensor

Inafanya kazi kwa kumulika mwanga katika kidole chako ili iweze kusoma alama za vidole kuzingatia uwazi katika pikseli za display ya OLED. Kuna uwezekano wa kwamba Synaptics na Samsung zilikuwa zinashirikiana kuleta teknolojia hii kwenye simu ya Galaxy S8, mwaka jana, mpaka walipogundua haitakuwa tayari kwa wakati wa kutolewa kwa simu.

Je nini maoni yako kuhusu teknolojia, tuambie mawazo yako hapa chini