WeChat yafikisha akaunti bilioni 1 dunia nzima

687
wechat-1bilioni

Mtandao wa kijamii kutoka China, WeChat, ambao hutumiwa kwa kila kitu kutoka kuzungumza na marafiki, kukata tiketi za kusafiria na kufanya malipo, umefikia akaunti za watumiaji bilioni 1 duniani.

Imeripotiwa na mtandao wa Financial Times. Idadi kubwa ya akaunti inaonyesha kutawala kwa programu hiyo, ingawa ni muhimu kukumbuka hii ina maanisha idadi ya akaunti na si idadi ya watumiaji. Watumiaji wanaweza kujiandikisha kwa akaunti zaidi ya moja, mfano wanaweza kufungua akaunti kwa ajili ya kazi na moja kwa matumizi binafsi.

Soma pia: WhatsApp imezuiwa matumizi nchini China, orodha ya mitandao ni zaidi ya 3,000 imezuiwa hadi sasa

Akaunti za watumiaji wa WeChat zilikua kwa asilimia 15.8 kwa mwaka, Tencent, kampuni ambayo inamiliki WeChat, iliripotiwa mnamo Septemba. WeChat ina watumiaji wa kila siku milioni 902, na jumbe karibu bilioni 38 hutumwa kila siku kwenye programu hiyo.