Wezi waiba iPhone zenye thamani ya $19,000 kwenye duka la Apple

115
wezi-iphone

Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, kikundi cha wezi waliiba iPhones zenye thamani ya Dola 19,000 (TZS 43 milioni) kutoka kwenye duka la Apple huko New York mwishoni mwa wiki iliyopita. Wanaume watano walionekana kwenye kamera za ndani za video(CCTV) kwenye ufuatiliaji wakati wa Tukio hilo katika store ya Huntington. Polisi wanatoa $5,000 kwa mtu yeyote ambaye ana habari itakayopelekea kukamatwa kwa wahalifu hao.

SOMA PIA: KENYA: Itaanza kutumia maputo ya Google kusambaza huduma ya internet vijijini

Shambulio hilo lilianza wakati watu watano waliingia kwenye duka na kuanza kutembea kwa kawaida kwa dakika chache. Muda mfupi baada ya hapo, walianza kuinua simu za iPhone 8 na iPhone X kutoka kwenye display counters za kabla ya kukimbia eneo hilo. Tukio hilo lililotokea saa 20:20 ya Ijumaa iliyopita.

Video fupi ya tukio zima:

Je nini maoni yako kuhusu hili. Tuambie hapo chini.