WhatsApp Business sasa inapatikana, ni maalum kwa biashara

830

WhatsApp wameleta programu nyingine mpya maalum kwa wafanya biashara, itakayo saidia mawasialiano kati ya kampuni na wateja wako

WhatsApp business inakupa sehemu ya kujaza profile ya biashara yako kama mahali ofisi zipo, muda wa kazi, barua pepe, huduma za biashara na tovuti yako. Pia utaweza kutengeneza ujumbe mfupi wa kujibu haraka au salamu, na kupata vipimo vya ni ujumbe upi umepokelewa na upi umesomwa.

Pia baada ya muda fulani, ‘Account’ za biashara zilivokua na uhakika zitapewa nembo ya kijani kuonyesha kwamba zipo ‘official’. WhatsApp business inapatikana kwenye nchi chache kwa sasa ambazo ni Indonesia, Italy, Mexico, UK na US, wiki zijazo itaachiwa kwa dunia nzima.

Soma Pia:

1. Instagram sasa yaruhusu watu wawili kwenda mubashara ‘Live’ kwa wakati mmoja

2. Maujuzi: Jinsi ya kuangalia movie mtandaoni bila kuipakua

Utumiaji wake hauna malipo yeyote, kwa wafanya biashara hii WhatsApp business itafaa. Kwa sasa WhatsApp Business inapatikana kwenye simu janja za Android pekee. Pakua WhatsApp Business

Tuachie maoni yako