WhatsApp imezuiwa matumizi nchini China, orodha ya mitandao ni zaidi ya 3,000 imezuiwa hadi sasa

844

Watumiaji wa programu ya kirusha ujumbe ‘WhatsApp’ wameshuhudia matatizo ya kutoweza kutuma picha na video au ujumbe wa aina yeyote kwenye programu hiyo, hadi ilipofahamika ni serikali ya China imekata mawasiliano ya programu hiyo.

 

China ni nchi ambayo imezuia programu nyingi kutumika, ambazo zinatambulika kila kona ya dunia kama Instagram, Facebook, Google, Gmail, Youtube, Twitter, Dropbox, Soundcloud na nyingine nyingi. Soma orodha ya mitandao yote

Google yakubali kununua sehemu ya HTC kwa dola bil 1.1

Kuzuiwa huko kumefanya watumiaji wengi kuhamia kwenye program ya WeChat, inasemekana mitandao kama Google, Facebook na WhatsApp zinakataa kuonyesha taarifa za watumiaje wake kwa serikali ya China, hii inawapa serikali ugumu kwenye mambo ya usalama wa nchi.

 

2 COMMENTS

Comments are closed.