WHATSAPP: Sasa utaweza kufuta ujumbe uliyotuma kama umekosea

858

WhatsApp imeamua kuleta kionjo kipya cha kuwapa watumiaji bilioni moja na zaidi uwezo wa kufuta ujumbe uliyotumwa kwa kukosea

Hapo mwanzo ilikua ni kufuta ujumbe kwenye simu yako lakini aliyepokea bado alikua na ujumbe wako. Ili kusuaidia watu waliokosea kutuma sasa uta bonyeza kitufe cha ‘Delete’ na utaletewa uchaguzi wa ‘Delete for everyone’

Soma pia:

  1. Hyatt: Shirika kubwa la hoteli duniani limeibiwa data za malipo(Visa card & Mastercard) na wadukuzu
  2. Instagram sasa yaruhusu watu wawili kwenda mubashara ‘Live’ kwa wakati mmoja

Kionjo hiki bado hakipatikani kwa kila mtu, lakini inasemekana kuwa ndani ya wiki ijayo itaanza kupatikana. Kwa sasa ukiwa na kionjo hiko na uliyemtumia ujumbe bado hana, ukifuta ujumbe wako hautafutika kwa mtumiaji ambae hana kionjo hiko. Kusoma zaidi kuhusu kionjo hicho tembea Q&A za WhatsApp kupata maelezo zaidi.