WhatsApp: Wameleta kionjo cha kufuatilia safari ya mtu kwa ‘Live – location’

947

Wiki iliyopita kampuni ya WhatsApp wameweza kuleta kionjo hicho kinacho kuruhusu kufatilia mahala rafiki yako alipo na anapoelekea kwa kuonyesha kwenye ramani muda huo huo (real time)

Live – location inakupa uchaguzi wa kufatilia rafiki yako kwa dakika 15, saa 1 au masaa 8 na kuzima baada ya muda kuisha.

Sasa utaweza kufatilia safari za watu kama ni kazi au mengineyo na kuona mwenendo wa kila mahali. Jinsi ya kutumia hiko kionjo ni kama ilivyoonyeshwa kwenye picha chini:

  1. Fungua mtu unaetaka kutumiana nae ujumbe mfupi na ‘Live – location’, baada ya hapo bofya kitufe cha ‘attach’ na chagua kitufe cha Location
  2. Itakuletea skrini ya kuonyesha ramani za maeneo uliyopo kwa muda huo, chini kutakua na kitufe cha ‘Share live location’, bofya kupata kionjo hicho.3. Utachagua muda ambao ungependa kufatiliwa na mtu utakae mtumia ramani yako, dakika 15, saa 1 au masaa 8, na kisha andika kichwa cha habari kuhusu safari yako.

Soma pia:

 

4. Tuma ujumbe wako, sasa atakua anafatilia ramani yako na kuona kila sehemu unayopita mpaka muda ulipoweka uish au uzuie wewe kwa kubofya kitufe cha ‘Stop sharing’

Baadhi ya watu hawajapenda kionjo hicho kwa kutopenda kufatiliwa na kutoa maoni yao kwenye mtandao wa kijamii Twitter. Ahsante kwa kusoma