WhatsApp ya Android kuja na vipengele hivi vipya

851

Wiki kadhaa zilizopita tuliona programu ya kutuma jumbe za papo kwa papo, WhatsApp ikipata kipengele kipya kinachojulikana kama ‘Delete for Everyone’ 

WhatsApp ya Android kuja na vipengele viwili (2) vipya
Tukiongelea programu za kutuma jumbe za papo kwa papo (Instant messaging), bila shaka WhatsApp inasimama katika nafasi ya kwanza. Sababu ya kwa nini watu wengi wanapendelea kutumia programu hii ni kua programu hii imekua ikifanyiwa mabadiliko mapya kila baada ya muda ili kuendana na wakati na mahitaji ya watumiaji wake.
Ni wiki kadhaa tu zimepita tangu tuone WhatsApp ikitambulisha kipengele chake kipya cha ‘Delete For Everyone’ kinachomuwezesha mtumiaji kuweza kufuta jumbe aliotuma ndani ya dakika 7.
Hivi karibuni taarifa kutoka WABetaInfo imetoa mwangaza wa vipengele viwili vipya kutoka kwa WhatsApp. Kipengele cha kwanza kitamuwezesha watumiaji kubadili kati ya simu ya sauti au video (voice na video call) kwa urahisi bila kukata simu iliyo hewani. Kipengele hiko kilikua kikionekana tangu mwezi July 2017.

Kipengele cha pili kitaruhusu mtumiaji kurekodi ujumbe wa sauti bila kushikilia kifungo cha kurekodi. Kwamba unaweza kuweka mikono yako huru wakati unarekodi ujumbe wa sauti. Watumiaji wanahitaji kuwasha kifungo cha lock ili kurekodi sauti. Vipengele vyote vilionekana kwenye WhatsApp kwa betas ya Android.
Tarehe ya uzinduzi ya wa vipengele hivi viwili bado haijatangazwa. Unafikiri nini kuhusu hili? Tuachie maoni yako katika sanduku la maoni hapa chini.