YOUTUBE: Jinsi ya kupakua video kutoka Youtube kwa simu janja na kompyuta zote

1174

Youtube imetengenezwa kwa ajili ya kuangalia video kwenye mtandao bila kuzipakua, na kutunza kwenye simu, diski ngumu au kompyuta. Kuna muda inakubidi utunze video fulani na hujui njia ya kupakua. Basi hii ni kwa ajili yako

Simu janja ya android

Tubemate ni programu nzuri na inayokidhi hitaji la kupakua video kwa wenye simu janja za android. Google hawapendi programu zote zinazopakua video kutoka Youtube kwa hiyo Tubemate haiwezi kuwepo kwenye Google Play, tembelea tovuti ya Tubemate kwa simu yako kupakua APK ya kuweka kwenye android.

Jinsi ya kutumia ni rahisi, baada ya kupakua bofya na uweze kuiweka kwenye programu za simu janja (Installing), ukiifungua baada ya kumaliza itakuletea  scrini yenye sehemu ya kuandika, andika link ya video ilipo kisha itafunguka na kuleta vionjo vya vya muonekano (quality) kuchagua kuhusu video hiyo

Simu janja ya iPhone

Ingia kwenye App Store na upakue programu janja inayoitwa Documents ni kwa ajili ya meneja ya mafaili ya simu janja za iPhone.

Jinsi ya kuitumia ni kwa kuingia kwenye video uliyoipenda kwa kivinjari cha Safari na bofya ‘share’ na copy hiyo link. Ingia kwenye programu ya Documents angalia kitufe chenye muonekano wa kivinjari, fungua tovuti ya savefrom.net na ‘paste’ ile link uliyocopy kutoka kwenye kivinjari cha Safari. Chagua ukubwa na muonekano utakaopendelea, baada ya hapo video itaweza kupatikana kwenye Documents, ihamishe kwenye kwenye Camera Roll.

Kompyuta yenye OS X au MacOs (Macbook au iMac)

hapa ni rahisi kwa utumie programu ya MacX YouTube Downloader. Baada ya kupakua programu hiyo ni kuweka link na kisha uchague ukubwa na muonekano. Pia unaweza kupata programu hiyo kwa wenye kompyuta za Windows hapa

 

Soma Pia:

 

Kompyuta yenye Windows

hapa zipo nyingi sana, ni upendeleo wako mwenyewe ipi itakufaa , IDM ni nzuri kuliko zote kutokana na urahisi wake ila itakupa siku 30 za kuitumia bure na kuomba malipo (crack zipo nyingi). kuangalia orodha ya programu zote  tembea tovuti hii

Sasa ni muda wako kutumia maujanja hayo niliyokupa, na kama unaswali usisite kuuliza nitakujibu. Ahsante