ZTE wazindua simu janja mpya yenye uwezo wa kujikunja

859

Kampuni ya simu ZTE hapo wiki iliyopita ilizindua simu janja mpya, Axon M. Simu janja hiyo ina skrini mbili ambazo zimegawanywa katika pande mbili na kuipa uwezo wa kujikunja kati kati.

Skrini mbili za Axon M zinaweza kukunjwa na kufanya kuwa simu yenye pande mbili za skrini (mbele na nyuma), na pia inaweza kukunjuliwa kama kitabu na kuwa na skrini mbili kwa upana.

Soma Pia: KRACK: Taarifa yatolewa simu janja hasa Android na kompyuta zote zenye Wi-Fi zipo hatarini

Taarifa zimesema kuwa muundo wa simu janja hiyo mpya sio wa kwanza na tayari tetesi zimesema kuwa Samsung pia walikuwa wakiufanyia kazi muundo kama huo kabla ya Galazy S8 kuzinduliwa.